Amani

Posted: 09/08/2012 in Uncategorized

Ingawa wiki bado changa, kuna mambo yanayoendelea kichinichini na watu hawaoni yanapofanyika katika kundi hili letu tulipendalo, kwa mfano, kuna tishio ya mlipuko wa uhusiano na amani ambayo imekuwepo kutoka mkufunzi mkongwe na mchezaji maarufu wa kitambo Kenny Dalglish kufutwa kazi, munaweza kukumbuka kwamba mfalme kenny alipokua mkufunzi na matokeo hayakua yanakwenda sambamba kulikuwepo na vikundi viwili vilivyoleta utata mkali kupindukia huku kundi moja likiongozwa na Xavier Lutta likitaka anyanganywe mamlaka ilhali upande ule mwingine wa mashabiki wa kenny ukiongozwa na Suso Pelosi Kariuki, mimi nakubali kwamba nilikua maarufu sana na shabiki wa mfalme. yote hayo yalikwisha Mfalme alipotimuliwa ikaonekana kwamba wanakundi wa LSCK(O) wataangalia mbele na waendelee kujenga kundi lao kama jamii. Haya yote yamepata tisho pindi tu mchezo wa kwanza wa kufungulia msimu huu ulipochezwa na wachezaji wakaonekana kua bado wana ulegevu na uchovu(inasemekana inaweza kuwa ni kwa sababu ya mazoezi mazito waliyopata walipokua wakijitayarishia msimu mpya), wachezaji wenyewe pia walionekana kulemewa na timu ndogo kutoka nchi ya Belarus. Isitoshe, matajiri wanaomiliki timu yetu tuipendayo iliyotuleta pamoja kwenye kundi hili hawaonekani kama wako tayari kutupa hela kama msimu uliopita maana pesa zao zilitumika kununua wachezaji wasiokua na uwezo wa kuitoa timu yetu kwenye msitu huu uliojitumbukiza. Nyufa zimeanza kujitokeza na dirisha la wachezaji wa kuhama matimu bado una siku ishirini na mbili na inatarajiwa kwamba mkufunzi mpya aliye kileleni Bw.brendan Rodgers ataweza kununua wachezaji watakaosisimua damu kama uvumi wa akina Xavier Lutta, Kelvin Suarez Oyugi, Suso Pelosi, Ramzy na wengineo wanaozidi kutuarifu kuwa wachezaji shupavu kama Clint dempsey, Gaston Ramirez, Theo Walcott,Ibrahim Affelay na wengineo waliokua wanahusishwa na kuhamia liverpool kutoka vilabu ambayo wanazochezea. Amani ni kitu muhimu sana(si wahu) katika kundi hililetu la LSCK na ustaarabu pia unahitajika. Huwa inafurahisha kupata watu wanabishana kwa uzuri kuhusu wachezaji ama kwa maoni yake, lakini sio vizuri kumlazimishia mtu awe na maoni kama yako, inasikitisha kuona watu wanatukanana ama kukasirikiana. Baba Ibrahim(father abraham) Sam Wanjere na نور إبراهيم huwa hawana utata wowote na hili ni jambo linalofurahisha maana huwa wanatupa masomo mazuri kuhusu kilabu chetu tukipendacho. Ni hayo machache niliyo nayo kwa leo. Bright Nunoo….. use google translator, hahaha. ~assalam aleykum~ El-torros Risas’ndani(bulletin)

Advertisements
Comments
  1. Alco says:

    Moha this is hard…

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s